MWERA AMAZING BLOG

MWERA AMAZING BLOG

MA-BLOGGER WOTE NCHINI TANZANIA HAKUNA KUTUMA HABARI AU PICHA YA MAADHIMISHO YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI NCHINI

index
Taarifa kwa Blogger wote nchini......
Chama cha Wamiliki/Waendeshaji wa Mitandao ya Jamii nchini ‘Tanzania Bloggers Network’ – TBN inawaomba wanachama wake wote kutotumia taarifa ama habari au picha yoyote kutoka katika mkutano wa maadhimisho ya Uhuru wa Vyombo vya Habari (WPFD) unaofanyika kitaifa mkoani Mwanza.
Kamati Kuu ya Uongozi TBN imefikia hatua hiyo leo baada ya kujadiliana na kujiridhisha kuwa kumekuwepo na taasisi za tasnia ya habari ambazo zimekuwa zikiwatenga wanahabari wa mitandao ya kijamii (bloggers) na kutotambua umuhimu wao wakati sehemu kubwa ya taarifa mbalimbali nchini husambazwa na mitandao hiyo.
TBN iliyosajiliwa rasmi serikalini Aprili 2015 na kupewa namba ya usajili; S. A 20008 inawataka wanachama wake kutotoa ushirikiano wa sina yoyote kwa taasisi ambazo zinawatenga bloggers.
Tunasikitika kufikia hatua hii ila hamna jinsi. TBN itasikitika na kumshangaa mwanachama wake au blogger asiye mwanachama kutounga mkono agizo hili, na kwenda kinyume na agizo hili. Muda umefika ‘Bloggers’ kudai heshima, kutambulika na kuthaminika kama tasnia ya habari ingine yoyote.
Share on Google Plus

About MWERA AMAZING

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Post a Comment