MWERA AMAZING BLOG

MWERA AMAZING BLOG

Moyes awaonya mashabiki wa Sunderland

David MoyesImage copyrightGETTY IMAGES
Image captionDavid Moyes
Meneja wa Sunderland David Moyes amewambia mashabiki wa klabu hiyo kujitayarisha kwa makabiliano ya kushushwa daraja msimu huu baada ya kushindwa mabao mawili kwa moja na Middlesbrough siku ya Jumapili.
Paka hao weusi wamepoteza mechi zao mbili za kwanza chini ya meneja Moyes ambaye alichukua nafasi ya Sam Allardyce ambaye ni meneja mpya wa England msimu huu.
Moyes aliongeza: 'Sidhani naweza kuficha ukweli. Watu watabaki hoi kwa sababu wanamatumaini kwamba kila kitu kitabadilika kimiujiza-haiwezi kubadilika na haitabadilika.'
Mechi ya Sunderland dhidi ya MiddlesbroughImage copyrightGETTY IMAGES
Image captionMechi ya Sunderland dhidi ya Middlesbrough
Klabu ya Sunderland katika misimu mine wamemaliza katika nafasi ya 17, 14, 16 na 17 mtawalia.
Kampeini za mwaka 2010-11 ndio mara ya mwisho ambapo klabu hiyo haikubadilisha meneja katika msimu huo.
Meneja Steve Bruce, Martin O'Neill, Paolo di Canio, Gus Poyet, Dick Advocaat na Allardyce wote wamewajibika kwa klabu hiyo kwa misimu mitano iliyopita.
Share on Google Plus

About MWERA AMAZING

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Post a Comment