MWERA AMAZING BLOG

MWERA AMAZING BLOG

Washambuliaji waua watu saba ufukweni

Washambuliaji wawili waliuawa na mmoja akakamatwa, polisi wa Somalia wamesemaImage copyrightEPA
Image captionWashambuliaji wawili waliuawa na mmoja akakamatwa, polisi wa Somalia wamesema
Watu wenye silaha wameshambulia mgahawa mmoja wa ufukweni mjini Mogadishu na kuwaua watu saba.
Shambulio lilianza kwa mlipuko wa bomu la kutegwa kwenye gari nje kidogo ya mgahawa wa Beach Club in eneo la Lido.
Baadaye, kulitokea ufyatulianaji mkali wa risasi.
Polisi wanasema washambuliaji wawili waliuawa wakati wa shambulio hilo lililotekelewa Alhamisi jioni.
Mshambuliaji wa tatu amejeruhiwa na anakamatwa.
Kundi la wapiganaji wa Kiislamu la Al Shabaab hutekeleza mashambulio ya moja kwa moja Mogadishu na maeneo mengine ya Somalia.
Mapema mwaka huu, watu 17 walifariki baada ya wapiganaji wa Al Shabaab kushambulia mgahawa mwingine katika ufukwe wa Lido.

kutoka BBC Swahili
Share on Google Plus

About MWERA AMAZING

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Post a Comment