
Cesc Fabregas
alifunga mabao mawili muda wa ziada na kusaidia Chelsea kujikwamua na
kulaza Leicester City katika mechi ya raundi ya tatu Kombe la Ligi
(EFL).
Muda mfupi kabla ya mapumziko, Chelsea walikuwa 2-0 nyuma kutokana na mabao ya Shinji Okazaki dakika ya 17 na 34 lakini Gary Cahill alikomboa moja muda mfupi kabla ya kipenga cha mapumziko kupulizwa.
Cesar Azpilicueta alisawazisha kwa kombora la mbali dakika ya 49.
Fabregas, 29, aliwaweka mbele kwa bao alilofunga dakika ya 92 kabla ya kuongeza jingine dakika ya 94.
Wasilewski alioneshwa kadi ya pili ya njano kwa kumgonga kwa kiwiko cha mkono mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa.
0 maoni:
Post a Comment