Marekani imesema ndege za kivita za
Urusi zilihusika kushambulia msafara wa misaada nchini Syria siku ya
Jumatatu na kusababisha vifo.
Maafisa wa Marekani wameiambia BBC
ndege mbili za kivita za Urusi aina ya SU-24, zilikuwa angani, sambamba
na msafara huo wa magari, wakati tukio hilo likitokea.
Hata hivyo Urusi imekana na kusema kuwa ndege hizo hazikuwa zake wala za Syria, na kutupia lawama wapiganaji wa waasi.
Wizara
ya Ulinzi ya Urusi imesema ndege zake zinazojiendesha zenyewe zilikuwa
zikifuatilia msafara huo, lakini kamera zao zilijizima kabla ya
mashambulizi kuanza.
Shambulio hilo la Jumatatu lilifanyika saa kadhaa baada ya serikali ya Syria kutangaza kumaliza wiki ya kusitisha mapigano.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 maoni:
Post a Comment