List ya kwanza ya wasanii watakaopanda kwenye steji ya SoundCityMVP2016 ni pamoja na Davido, Patoranking, Tekno, na Olamide huku mshereheshaji wa siku usiku huo atakuwa ni Bright Okpocha a.k.a Basketmouth, comedian kutoka Nigeria.
Kwa mujibu wa waandaji wa tuzo hizo wameeleza kuwa list ya wasanii watakaoperform siku hiyo itakuwa na mastaa kutoka Tanzania, South Africa na Nigeria ambao wataonekana live kutoka kwenye ukumbi wa Expo Center, Eko Hotel & Suites jijini Lagos, Nigeria.
Inaelezwa kwamba zaidi ya watazamaji milioni 50 kutoka Afrika watashuhudia utoaji wa tuzo hizo kwa njia ya TV pamoja na wale watakaokuwa live ukumbini. Tuzo hizi zinatarajiwa kutolewa tarehe 29 December, na unaweza kuwapigia kura wasanii kutoka Tanzania kwa kuingia hapa soundcitymvp.com.
kutoka Millardayo.com
0 maoni:
Post a Comment