Idara ya jeshi nchini Marekani kwa
mara ya kwanza itajaribu kudungua kombora la masafa marefu lililo na
uwezo wa kufyatuliwa kutoka bara moja hadi bara lingine.
Kumekuwa na wasiwasi mjini Washington kuhusu uboreshaji wa miradi ya kinyuklia na makombora ya masafa marefu ya Korea Kaskazini.
Mkuu wa shirika la ujasusi la Marekani anasema iwapo miradi ya Korea Kaskazini ya kutengeneza makombora haitodhibitiwa, basi taifa hilo lina uwezo wa kutengeneza kombora lenye uwezo wa kufikia Marekani.
Kutoka BBC Swahili.com
0 maoni:
Post a Comment