Viongozi kadha wa nchi za Afrika
wanahudhuria siku ya pili ya mazungumzo katika mkutano huo wa G7, ili
kujadili tatizo la wahamiaji.
Tayari mwaka huu, wahamiaji elfu hamsini wameingia Italia, huku 1500 wamezama safarini.
Kwa hivyo viongozi wa G7 wamezungumza na wenzao kutoka Tunisia, Kenya, Ethiopia, Niger na Nigeria, kutafuta njia za kuhimiza maendeleo Afrika, ikitarajiwa kuwa itawafanya wahamiaji wabaki makwao.
Lakini juhudi za Itali, za kutaka G7 kukubali kupokea wahamiaji zaidi, inaelekea zitapingwa na hasa Marekani.
kutoka BBC Swahili
0 maoni:
Post a Comment