Rais wa Marekani Barack Obama,
amesema uvumilivu na ujasiri wa Nelson Mandela ni mfano mwema kwa dunia na
upendo wa dhati wa rais huyo wa zamani wa taifa la Afrika Kusini inaonyesha ni
kwa namna gani alivyo na utu wa kibinadamu.
Bwana Obama ameongeza kuwa Mandela, alionyesha ukweli na ukakamavu ambao una maana kubwa katika utu wa kibinadamu ambao uliondoa tabaka la ubaguzi, udini na utaifa.
Rais huyo wa marekani ameyazungumza hayo mjini Pretoria baada ya mazungumzo na rais wa sasa wa Afrika kusini, Jacob Zuma.
0 maoni:
Post a Comment