Msanii wa Bongo Fleva, Ally Kiba, ndiye msanii pekee
anayeshika chati nchini Oman, hayo ni kwa mujibu wa mmoja ya watanzania
anayeishi nchini Humo.
Mtandao wa Bongo5, umeandika hayo kutokana na
maongezi waliyoyafanya na mtazania huyo kwa njia ya mtandao, mTz
huyo alijulikana kwa jina la Rayya Al Habsi, aliiambia Bongo5, kuwa
mziki wa Bongo fleva unamashabiki wengi nchini humo ata na watu wasiojua Kiswahili
kabisa.
Pia aliwattaja wasanii ambao wanashika chati nchini
humo ni pamoja na Ally Kiba, Ommy Dimpoz
na Dully Sykes, sambamba na kundi la Off Side Trick, AT, na Kilimanjaro
Band.
Aliendelea kufunguka na kusema kuwa wasanii wengi wa
Hip Hop, hawana majina kabisa nchini humo.
0 maoni:
Post a Comment