wa Hip Hop nchini Tanzania, Madee, amefunguka
kilichomtokea nchini Afrika Kusini, anasema kuwa alipojulikana kuwa ni
mtanzania, alishikiliwa na kushukiwa kuwa nay eye ni miongoni mwa wadau.
Madee alisema kuwa
alipotua kwenye kiwanja cha ndege, kawaida huwa kuna utaratibu wa kuchekiwa
hati ya kusafiria na ukaguzi mwingine ambao hufanywa na mitambo maalum kwa kila
abiria anaeingia Afrika kusini, ni ukaguzi ambao unafanywa Airport kabla ya
abiria kuruhusiwa kuingia kwenye nchi yenyewe.
Kilichomfanya Madee
kusachiwa na kuhojiwa karibu dakika 60 ni pale tu aliposema anatokea Tanzania,
kuna wazungu wawili wenye sare tofauti za kipolisi wakaanza kumsachi mpaka
kufikia kumwambia avue t shirt yake, alivua t shirt na kubakiwa na nguo nyepesi
ya ndani wakati huo abiria wenzake aliokwenda nao walikua wameruhusiwa.
Hayo aliyasema
msanii huyo wakati alipokuwa anafanyiwa interview na mtandao wa millardayo.com,
yote hayo ni kutokana na kile cha watanzania wachache kukamatwa na madawa ya
kulevya nchini humo.
0 maoni:
Post a Comment