MANENO KUTOKA KWA MILLARD AYO
Huku tunakoishi uswahilini wengi wetu huwa hata majumba ya Cinema wanakolipia elfu kumi kutazama movie huwa hatuyafahamu au hatujawahi kwenda kabisa…. hivyo kuna kautaratibu ketu ka kuchangisha hizi mia mia na mia mbili kwa ajili ya kuingia ‘vibanda umiza’ ambavyo huwa vinatutoza hizo senti kwa ajili ya kutazama movie zilizotafsiriwa pamoja na mpira…. yani kutazama hivyo vitu viwili sehemu kama hizo ni kawaida kabisa.
Sasa bwana kwenye eneo la Kisarawe ambalo liko kwenye mkoa wa Pwani, kuna mjanja mmoja alitumia akili ya ziada kujua kwamba sio kila mmoja anaweza kwenda town kusubiria kuona msafara wa Rais Obama, hivyo akaamua kuchangisha hizo mia mia kwa kila anaetaka kutazama ujio wa Rais Barack Obama Tanzania ambao ulikua unaonyeshwa moja kwa moja na vituo mbalimbali vya TV ikiwemo ya Taifa TBC1 na Clouds TV.
Uhakika wa kuzikusanya hizo mia mia ulikuwepo sana kwa sababu kwanza Kisarawe sio kila Mwananchi anamiliki TV au nyumba yake ina umeme hivyo ni lazima tu kama angekua na shilingi 100 angejikusanya kwenye kibanda umiza kucheki hilo movie la Obama kwenye ardhi ya Tanzania
kutoka kwa Millard ayo.com
0 maoni:
Post a Comment