Rais wa Marekani Barack Obama,
amewasili nchini Tanzania katika mkondo wake wa mwisho wa ziara yake barani
Afrika.
Ziara ya Obama inasemekana kulenga
kuimarisha uhusiano wa kibiashara na Afrika huku kukiwa na wasiwasi kuwa
Marekani inaachwa nyuma na China katika uhusiano wao na Afrika.
Obama amewasili Tanzania baada ya ziara
yake ya Afrika Kusini ambako rais mstaafu Nelson Mandela anaugua.
Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete na
familia yake pamoja na maafisa wake wa serikali na wacheza densi za kitamaduni
walimkaribisha Obama na familia yake mjini Dar es Salaam.
Baadhi ya wananchi wa Tanzania
kupitia mitandao ya kijamii wamekosoa ziara ya Obama katika nchi yao, wakisema
kuwa ziara yake imeathiri shughuli za maisha yao ya kila siku.
Obama alitembelea Senegal kabla ya
kupitia Afrika Kusini na kisha Tanzania ambako ziara yake ya Afrika inaishia
kabla ya kurejea Marekani.
Obama ameambatana mamia ya
wafanyabiashara na swala la uchumi linatarajiwa kupewa kipamboele kwenye
ajenda.
Aidha Obama atatembelea kiwanda cha
kuzalisha umeme kinachomilikiwa na Marekani kufuatia tangazo lake mwishoni mwa
wiki wa mpango wa mabilioni ya dola kufadhili mradi wa uzalishaji wa kawi.
Mpango huo wa miaka mitano,
unatarajiwa kuwezesha nchi nyingi Afrika kuweza kupata kawi kwa ushrikiano na
nchi zingine za Afrika na sekta binafsi.
Wakati wa ziara yake, nchini Afrika
Kusini, kiongozi huyo wa Marekani hakumtembelea Mandela ambaye anasalia kuwa
mahututi hospitalini akiigua maradhi ya mapafu.
Duru zinasema kuwa barabara
zimefungwa na usalama kudhibitiwa vilivyo, mjini Dar es Salaam.
0 maoni:
Post a Comment