Kundi la M23, la nchini Congo, Ladaiwa kuwaua watu
zaidi ya 40, na kuwabaka wasichana na wanawake takwimu hiyo ni kutokana na
shirika la kutetea haki za Binadamu la Human Rights Watch.
Shirika hilo limedai kuwa waasi hao wanawasajili
vijana kinguvu wengi wao wakiwa kutoka nchini Congo na wengine Rwanda, hili
wajiunge na kundi hilo.
Pia inasemekana kuwa Jeshi la Rwanda bado linawapa
nguvu kundi hilo ingawaje Serikali ya nchi hiyo inapinga madai hayo.
Jeshi la Congo lilishambulia Ngome ya Waasi, hikiwa
ni mara ya kwanza kwa hjeshi hilo kushambulia waasi hao, tokea kuanza kwa
mapigano kati ya pande hizo mbili.
0 maoni:
Post a Comment