Katika siku ya tatu ya kesi ya
mwanasiasa mashuhuri wa Uchina, Bo Xilai, mshtakiwa ameutoa maanani ushahidi
dhidi yake kuhusu madai ya ufisadi yanayomkabili.
Shahidi mmoja amesema alimuona Bwana Bo
akimwambia mkewe achukue hongo ya dola 800,000 kutoka mradi wa majenzi wa mji
wa Dalian, ambako mwanasiasa huyo aliwahi kuwa meya.
Lakini Bo alisema kuwa ni mtu mpumbavu
pekee anayezungumza swala la rushwa mbele ya mashahidi.
Maelezo ya kesi hiyo yanaendelea kuwekwa
katika mtandao wa Weibo nchini humo.
Mwandishi wa BBC anasema inachukuliwa
kuwa Bwana Bo atapatikana na hatia, kwa sababu umaarufu wake na hamu yake ya
madaraka ukitishia viongozi wenzake wa chama cha kikoministi.
Mahakama hiyo bado haijaangazia shtaka
la utumizi mbaya wa wadhifa.
Bwana Bo ameshtakiwa kwa kufunika
kuhusika kwa mkewe katika mauaji ya mfanyabiashara mmoja kutoka Uingereza.
Kutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment