Msanii wa muziki nchini, Diamond Platnumz, ametumia
kiasi kikubwa katika kurekodi video ya nyimbo yake mpya, gharama ya nyimbo hiyo
ambayo imefanyiwa nchini Afrika Kusini ni sawa na Dolla 30,000, ni zaidi ya mil
50, za kitanzania.
Msanii huyo alifunguka na kusema kuwa wimbo huo
utaachiliwa hivi karibuni katika Radio mbalimbali za hapa nchini na nje ya
nchi, aliendelea kwa kusema kuwa “ siku zote mimi ni muumini wa vitu vizuri,
nimegharamia wimbo wangu sasa nakuja kuwakamata mashabiki wangu kwa namba moja,
hii ni ngoma nimerekodi Afrika Kusini” hayo yalikuwa maneno ya Diamond wakati
akifanyiwa mahojiano na Gazeti la Mtanzania.
0 maoni:
Post a Comment