Serikali ya Kenya kupitia kwa waziri wake wa usalama Joseph Ole Lenku
imesema kuwa watu 59 wamefariki katika shambulizi la kigaidi lililofanywa na
wanamgambo wa Al Shabaab na wengine 175 kujeruhiwa.
Waziri Ole Lenku amesema kuwa idadi ya magaidi walio ndani ya
jengo hilo ni kati ya kumi na kumi na tano na haijulikani ikiwa wanwazulia
waathiriwa au waathiriwa wamjificha katika sehemu mbali mbali z jumba la
Westgate.
Shirika la Red Cross awali katika taarifa yake ilisema kuwa watu
43 ndio waliofariki na zaidi ya 50 kujeruhiwa huku wengine wakitekwa nyara
katika mashambulizi la kigaidi Jumamosi mchana.
Milio ya risasi imeweza kusikika katika jengo la Westgate mjini
Nairobi Kenya, ambako wanamgambo wa Al shabaab wanawazuilia mateka ambao idadi
yao haijajulikana hadi sasa.
0 maoni:
Post a Comment