Msanii
wa zamani wa kundi la Daz Nundaz, ambaye ni Daz Baba, amechanganyikiwa kutokana
na mambo aliyoyafanya hivi karibuni, ambayo hayawezi kufanywa na mtu mwenye
hakili zake.
Daz Baba, alionekana maeneo ya Morogoro, akiwa
katika hali ya kushangaza zaidi, iliyopelekea wadau wengi na mashabiki wa
muziki kushangazwa na hali hiyo. Rafiki wa karibu wa msanii huyo alizungumza na
Bongo 5, hapo jana na kusema kuwa msanii huyo kwa sasa amechanganyikiwa na
anakila dalili ya kuwa mtu aliyechanganyikiwa pia amekuwa mtu wa kuzunguka
Barabarani huku akiwa anafanya matukio ya hajabu.
Inasemekana kuwa hivi karibuni msanii huyo alikwenda
nyumbani kwa Afande Sele, mida ya usiku huku akiwa anapiga kelele sana, afande
alitoka na kumkuta Daz Baba, akiwa mchafu sana na akiongea maneno
yasiyoeleweka, sambamba na kutaka kumfanyia kitu kibaya mfanyakazi wa ndani wa
afande sele, lakini hakufanikiwa na watu wakajua kuwa mwana ameshadata.
Hayo yote yalithibitishwa na Afande Sele, mara baada
ya kufanyiwa mahojiano na mtandao wa Bongo 5, Pia alisema kuwa ameshampa
taarifa Dada yake wa Dar es salaam,
Afande alifunguka na kusema kuwa “ kweli hali ya
Daz, ni mbaya tena mbaya, nimejaribu kumuweka sawa lakini nimeshindwa labda
wakamfanyie matambiko ya kwao kwasababu Baba na Mama yake walifariki na
walikuwa hawaelewani labda kuna matatizo ya kifamilia” alisema Afande Sele.
0 maoni:
Post a Comment