Liverpool imejiweka katika nafasi nzuri sana kwenye ligi ya
Uingereza baada ya kuwazima mabingwa wa ligi hiyo Manchester United kwa bao
moja kwa bila katika uwanja wa Anfield.
Hii ni mara ya kwanza kabisa kwa
Liverpool kuwa katika nasafi kama hii mwanzo mwanzo wa ligi tangu mwaka 1995.
Pia Liverpool inakuwa timu ya kwanza
tangu mwaka 2011 kucheza mechi tatu mfululizo katika ligi hiyo bila ya kufungwa
goli lolote.
Ilikuwa fursa nzuri kwa kuhitimisha
miaka 24 tangu kuzaliwa kwa kuipatia Liverpool bao hilo la pekee na la ushindi.
Mwamba huyo alifunga bao hilo kwa
ustadi mkubwa kwani alifunga kwa kichwa safi ambapo kipa wa Man U De Gea
alishtukia wavu ukitikisika.
Ni mara ya tatu mfululizo kwa
Sturridge kuivungia timu yake tangu ligi hii ya Uingereza ianze.
Kushindwa kwa Manchester United
inachafua rekodi ya kocha wao mpya David Moyes kwani hata akiwa mkufunzi wa
Everton hajawahi kuingozi timu yake kuifunga Liverpool katika uwanja wa
Anfield.
Hata Robin van Persie alikuwa na
siku mbaya kwani alikuwa na wakati mgumu kumfunga kipa mpya wa Liverpool Simon
Mignolet, ambaye alizima ndoto ya Man U ya kupata bao.
Tangu mlinda lango huyo Mignolet,
kuhamia Anfield kutoka Sunderland kwa kima cha £9m hajafungwa bao hata moja.
0 maoni:
Post a Comment