MWERA AMAZING BLOG

MWERA AMAZING BLOG

MASOGANGE NA MELISSA WAKO HURU

Mwanadada Masogange kwa sasa ni mtu huru, ameachiliwa kuwa huru uko nchini Afrika Kusini mara baada ya kulipa faini ya shilingi milioni 4.8, mahakama ya nchini Afrika Kusini Imewachilia huru mwanadada huyo sambamba na mdogo wake baada ya kukosekana na hatia ya kubeba madawa ya kulevya.
Inasemekana kuwa mahakama imefutalia mbali kesi hiyo baada ya uchunguzi kufanyika na kugundua kuwa mdogo mtu hakuwa na kosa bali alikuwa akimsaidia Dada yake ambaye ni masogange, na madawa hayo hayakuwa ni madawa ya kulevya bali ni kemikali zinazotumika kutengenezea madawa hayo.
Masogange alitakiwa kufungwa kipindi cha miaka miwili au kulipa faini ya shilingi milioni 4.8, hivyo basi mzamini wake alilipa nusu ya pesa hizo na kuhaidi kumalizia deni kwa kipindi kifupi kijacho, hivyo basi mwadada huyo ataendelea kubaki nchini humo mpaka kumalizika kwa deni.
Hapo hawali ilibainika kuwa walikamatwa na madawa ya kulevya lakini mahakama ilisema kuwa hawakukutwa na madawa ya kulevya bali walikutwa na kemikali za kutengenezea madawa hayo, hiyo kukutwa na kemikali yoyote iliyokatwazwa nchini humo ni kosa la jinai.


Share on Google Plus

About MWERA AMAZING

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Post a Comment