Vikosi vya usalama nchini Kenya
vinasema viko katika mkondo wa lala salama katika kuweza kudhibiti jengo zima
la Westgate. Hadi sasa serikali inasema kuwa mateka wote wameokolewa huku
wanamgambo sita waliosalia wakiuawa usiku wa kuamkia leo.
Kwa mujibu wa taarifa za maafisa wa usalama idadi kamili ya
magaidi waliouawa ni tisa
Duru kutoka shirika la AFP zinasema kuwa
majeshi ya Kenya yangali yanakabiliana na gaidi mmoja au wawili ambao wamesalia
ndani ya jengo la Westgate.
Inaarifiwa magaidi hao walijitawanya wakiwa ndani ya jengo hilo
kila mmoja akijificha sehemu yake katika ghorofa ya juu zaidi ya jengo hilo.
Milio ya risasi na milipuko ilisikika mapema leo asubuhi kutoka
katika jengo hilo.
Ukabilianaji huo ulitokea baada ya
serikali ya Kenya kutangaza kudhibiti jengo hilo zima huku hali hiyo
ikishuhudiwa kwa siku ya nne.
Serikali ilisema kuwa mateka wote wameokolewa ingawa bado
haijatoa taarifa rasmi kuhusu hali ilivyo
Kutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment