Mshiriki wa BBA, kipindi cha miaka
kadhaa iliyopita, Mwisho Mwampamba, ambaye kwa sasa anaishi nchini Namibia,
amefunguka kupitia Facebook, na kusema kuwa Namibia ni nchi inayofanya ubaguzi
wa hali ya juu kabisa.
Mwisho
aliandika maneno haya yenye simanzi kubwa sana kwa kila Mtanzania, na kitu
kinachopelekea baadhi ya Watanzania kuichukia Namibia na Afrika Kusini kwa
kutufanyia Ubaguzi ingawaje wote ni mablack. ( kwakuwa Namibia Ipo HURU, naona
woga dhidi ya raia wa kigeni (xenophobia) imekuja kwa kasi. P;lisi walikuja
nyumbani kwangu na kuniambia natakiwa nirudi kwenye nchi yangu, manyanyaso
kwenye mpaka, Huwa Napata Visa ya Miezi miwili tu, licha ya kuwa SADC na nimeoa
Mnamibia, Swali langu ni , Mveterani wenu wote wametoka wapi ? Mnawatendea
wakoloni wenu wa zamani vizuri kuliko wakombozi wenu ? Huwa inafedhehesha kuona
jinsi Wanamibia na waafrika kusini walivyo.
Wanamibia
na waafrika Kusini wanatutendea sisi waafrika wengine kama nyani kwakuwa sasa
mko huru. Wamesahau mapema jinsi tulivyowasaidia japokuwa masikini na wenye njaa, ni sawa
tulifanya sababu kilikuwa ni kitu sahihi kufanya na sikupata fadhila yenu,
lakini tunatarajia walau heshima na kutendewa kama Binadam) Hayo yalikuwa
maneno ya mwisho, maneno yanatia uchungu sana na kuona jinsi gani Watanzania
Tunavyofanya ingawaje tumejawa na roho njema.
0 maoni:
Post a Comment