Akaunti ya Twitter ya kundi la wanamgambo wa Al
Shabaab imesitishwa kwa mara nyingine.
Ujumbe kutoka kwa
Twitter katika akaunti yake ya @HSMPress1 ulisema kuwa akaunti hiyo imefungwa,
ingawa hapakuwa na maelezo kwa nini hatua hiyo ilichukuliwa.
Katika taarifa
iliyotumwa kwa shirika la habari la AFP kundi hilo lililaani hatua ya Twitter
na kusema kuwa haitazaa matunda yoyote.
Mnamo siku ya Jumanne,
Al Shabaab ilisema kuwa ilishambulia msafara wa magari ya rais wa Somalia
Hassan Sheikh Mohamud, ambaye hakujeruhiwa.
Hata hivyo habari hizo
zilipuuzwa na ofisi yake ikisema kuwa rais hakujeruhiwa kwani kifaa kililipuka
mbali sana na msafara wake.
Baadaye kundi hilo
lilituma ujumbe kwa Twitter uliosema kuwa ,''Mara nyingine hautaponea ''kwa
mujibu wa ripoti za , AFP.
Hata hivyo akaunti
yake ya kiarabu ingali iko wazi.
Kwa mujibu wa sera ya
Twitter, akaunti zinazotumika kutuma vitisho,zinapaswa kufungwa. Akaunti pia
zinaweza kufungwa ikiwa zinatumiwa kwa shughuli zisizo halali.
Taarifa ya Al-Shabab
ilisema kuwa haina akaunti nyingine ya Twitter kwa kiingereza na kuwaonya
watumiaji wa mtandao
huo kuwa wajiandae kwa akaunti zao kuvamiwa.
Akaunti ya Twitter ya
kundi hilo kwa jina @HSMPress, ilisitishwa mwezi Januari baada ya kundi hilo
kuitumia kutuma ujumbe wa kutisha kuwa lingewaua mateka wa Kenya na kisha
kusema kuwa limefanya hivyo.
Wadadisi wamesema kuwa
katika siku za nyuma, Marekani ililazimisha Twitter kufunga akaunti hiyo ingawa
haikuwa na nguvu za kisheria kufanya hivyo.
Hata hivyo Twitter
inasema kuwa hakuna kitu kinachoweza kuzuia Al Shabaab kuwa na akunti nyingine
baada ya nyingine za kwanza kufungwa.
Al-Shabab ilifungua
akauti yake mara ya kwanza mwezi Disemba mwaka 2011 baada ya wanajeshi wa Kenya
, kwenda Somalia kupambana na wanamgambo hao.
Wanamgambo hao
wamefurushwa Mogadishu pamoja na kutoka miji mingine ingawa bado wanadhibiti
sehemu nyingi za Kusini mwa Somalia.
Kutoka BBC.
0 maoni:
Post a Comment