Miss World |
Makundi ya wanaharakati wa KiiSlamu
nchini Indonesia, yametishia kuyavamia mashindano ya Miss World 2013, yatakayofanyika
nchini humo katika kisiwa cha Bali.
Pia
makundi ya wanawake wa Kiislamu wamejitokeza na kuamdamana katika barabara na
kupinga mashindano hayo kufanyika katika nchi yao, moja ya makundi hayo
yameandamana katika visiwa vya Sumatra nchini humo siku chache zilizopita.
Waisilamu
nchini humo wamepanga kufanya maandamano mengine siku ya jumamosi ambayo ndiyo
siku ya shindano lenyewe pia wamesema kuwa watafanya mavamizi katika shindano
hilo na kuvishinda vikosi vya usalama vya nchi hiyo, asilimia kubwa ya watu
nchini humo ni waislamu.
Waandaaji
wa shindano hilo waliomba kuwa hawatowazisha washiriki vyazi la Bikini na
wakaendelea kusema kuwa watawavyesha nguo ndefu na zenye kuziba mwili mzima,
lakini bado walikuwa katika wakati mgumu kutokana na majibu ya waislamu kuwa
hawataki shindano hilo na walipeleke nchi nyengine lakini siyo nchini mwao.
Miss Indonesia |
Baadhi
ya mabarozi wan chi kadhaa wametia shaka na kusema kuwa shindano hilo uwenda
likavamiwa, pia walikumbushia kuwa mwaka 2012, kulikuwa na tukio la kujitoa
jihadi na bomu ambalo liliuwa watu 200.
Pia
kipindi cha mwaka uliopita msanii kutoka nchini Marekani, Lady Gaga, alishindwa
kufanya tamasha lake katika mji wa Jakarta, kutokana na maandamano ya kupinga tamasha
la Msanii huyo, baada ya kumuita kuwa ni mfuasi wa shetani anayevaa Chupi na
sidiria tu.
hivi ndivyo Miss Indonesia anavyokuwa akiwa kwenye jukwaa. |
Wanaharakati
hao walitaka kumzuia msanii huyo asishuke kwende ndege, na walitaka kuuchoma
ukumbi huo ambao angefanyia tamasha lake nchini humo.
Ulinzi
utakuwa wakutosha katika tamasha la Miss world kufuatia taarifa za kulivamia
tamasha hilo kupamba moto, walinzi 700, kilinda wageni na washiriki.
0 maoni:
Post a Comment