Maafisa katika kisiwa kikubwa cha Sicily katika bahari ya Meditarenia
wanasema kuwa wamepata maiti 130 baada ya mashua iliyokuwa imewabeba takriban
wahamiaji 500 wa kiafrika kushika moto na kuzama katika kisiwa cha Lampedusa.
Boti hiyo ilikuwa safarini kuelekea Ulaya lakini ikazama katika
kisiwa cha Lampedusa katika pwani ya Utaliana
Takriban miili 103 imepatikana baharini na mingine zaidi
kupatikana ndani ya boti iliyozama.
Inaarifiwa abiria walijirusha baharini wakati moto ulipozuka
ndani ya boti
Zaidi ya wahamiaji 150 wameokolewa.
Wengi wa wahamiaji hao walikuwa raia wa Eritrea na Somalia,kwa
mujibu wa Umoja wa Mataifa.
0 maoni:
Post a Comment