Ndege iliyokuwa imewabeba watu 27
imeanguka baada ya kukumbwa na hitilafu ya injini, muda mfupi baada ya kuruka
kutoka uwanja wa ndege mjini Lagos.
Duru zinasema kuwa watu 5 wamefariki huku shughuli ya uokozi
ikendelea na mtu mmoja akipata matibabu kwa majeraha mabaya aliyopata.
Ndege hiyo ya shirika la ndege la Associated Airlines, iliyokuwa
na uwezo wa kubeba watu 30 ilianguka muda mfupi tu baada ya kuruka na kulipuka.
Aidha ilikua inaelekea mjini Akure Kusini Magharibi mwa nchi,
kwa mujibu wa msemaji wa shirika la
udhibiti wa safari za angani nchini humo.
Injini ya ndege ilikumbwa na hitilafu na kuisababisha ndege
kuanguka na kuteketea.
Hata hivyo hakuna taarifa za kuthibitisha idadi ya watu
waliofariki.
Ndega hiyo iliruka mwendo wa saa mbili unusu kutoka katika
uwanja wa kimataifa wa ndege wa Murtala Mohammed
Maafisa walisema kuwa ndege hiyo ilianguka karibu na bomba la
mafuta katika uwanja huo.
Haijulikani ikiwa mafuta hayo ndiyo yalisababisha ndege
kulipuka.
Shahidi mmoja alimbia BBC kuwa alisikia mlipuko mkubwa
uliofatiwa na moshi mkubwa ukifuka kutoka katika sehemu ya ajali hiyo.
Maafisa wa usalama waliharakisha kwenda katika eneo la ajali na
kuanza kuwaokoa abiria wal
iokuwa ndani ya ndege hii
Usafiri wa ndege Nigeria
• Ajali kubwa saba za ndege tangu mwaka 1992
• Usalama katika sekta ya safari za ndege uliimarishwa mwaka
2007
• Mashirika yote ya ndege yalilazimika kujiimarisha upya la
sivyo yasimamishwe
• Mwezi Agosti mwaka 2010, Marekani iliipatia Nigeria hadhi ya
juu ya usalama na kuruhusu ndege zake kwenda moja kwa moja hadi Marekani
• Uwanja wa ndege wa Lagos Murtala Muhammed ni kitovu cha
usafiri Magharibi mwa Afrika huku abiria milioni 2.3 wakipita hapo kuanzia mwaka
2009
• Serikali ya Nigeria inasema kuwa inaweza kunasa safari za
ndege kwenye mfumo wa Radar kote nchini.
kutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment