Rais wa Tanzania , J.M. Kikwete |
Tanzania imesema
hataitajitoa katika Jumuiya ya Afrika kama
wengi walivyodhani na badala yake imedhamiria kuhakikisha Jumuiya hiyo inadumu
na kustawi.
Akilihutubia bunge la Tanzania, mjini Dodoma, katikati mwa Tanzania, Rais wa nchi hiyo, Jakaya Kikwete amesema kwamba Tanzania haina mpango wala fikra za kujitoa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kuwa ni nchi inayoamini katika umoja na maendeleo na imekuwa ikitumia gharama kubwa kuhakikisha jumuiya hiyo inaimarika.
"Tanzania ni mwanachama mvumilivu, mtiifu na mwaminifu na tunatimiza wajibu wetu kwa jumuiya na kuhusika kikamilifu katika ujenzi wake." amesema Rais Kikwete.
Rais Kikwete ametumia muda mrefu katika hotuba hiyo kuchambua masuala mbalimbali ya msingi ya uhai wa jumuiya hiyo huku akisema ameshangazwa na nchi za Kenya, Uganda na Rwanda kuzitenga Tanzania na Burundi.
Amesema kuna masuala ambayo hayazifungi nchi wanachama katika mkataba wa umoja wao, hivyo kuwa na uhuru wa ushirikiano na nchi ndani ya jumuiya na hata nje.
0 maoni:
Post a Comment