Utengenezaji wa filamu mpya ya Fast and
Furious utaendelea licha ya kifo cha mmoja wa mastaa wake, Paul Walker.
Utengenezaji wa filamu hiyo yenye bajeti kubwa ulikuwa umesimama weekend wakati
wa sikukuu ya Thanksgiving ambapo Walker
alipata ajali na kufa siku ya Jumamosi.
Walker alikuwa
arejee kuendelea na utengenezaji wa filamu hiyo jijini Atlanta nakuungana na mastaa wenzie Vin
Deisel na Dwayne Johnson aka The Rock.
James Wan, ambaye ni muongozaji wa
filamu hiyo na wakurugenzi kutoka Universal Studios walifanya mkutano jana
asubuhi kujadili jinsi ya kuendelea na Fast and Furious 7 katika njia ambayo
itakuwa na heshima kwa kifo cha Walker.
Kwa mujibu wa The Hollywood Reporter,
kushoot kunaweza kuanza Jumanne hii. Walker alikuwa akiigiza kama Brian
O'Conner, mhalifu aliyebadilika na kuwa polisi kwenye Fast and Furious 7,
uhusika alioucheza katika filamu sita zilizopita za Fast and Furious.
Shooting ya filamu hiyo itamalizka
Januariy huko Abu Dhabi.
[Imetoka timesfm]
0 maoni:
Post a Comment