MWERA AMAZING BLOG

MWERA AMAZING BLOG

DK. CHEKI, KUMBE ANACHOCHEA USHOGA !!!!!!!!!! LAKINI DK. HAKUNUSHA.



 DK Cheni adai filamu yake
Uamuzi wa bodi ya Filamu Tanzania (TFB) kuizuia filamu ya muigizaji wa kiume na mkongwe, Dk Cheni ‘Nimekubali Kuolewa’, kwa madai ya kukiuka maadili na kuchochea tabia za ushoga, umepingwa na msanii huyo ambaye anaamini kabisa kuwa maudhui ya filamu hiyo yangeelisha jamii zaidi ya picha katika cover yake.


Hapa alifunguka alipokuwa akiiambia Global Publisher “Eti ushoga wangu uko kwenye kujiremba sana, wamenionea, lengo letu ni kukemea na kupinga vikali vitendo vya ushoga na ndoa za jinsia moja, huwezi kuelimisha bila kuonesha madhara yake kwa vitendo kama ilivyo kwenye filamu hiyo. Amesema Dk Cheni.

Kupitia Tovuti ya Times fm, alifunguka na kusema kuwa “Nahisi filamu inayokuja inaitwa ‘Nimekubali Kuolewa’, itakuwa ya kipekee sana, kwa sababu hata pale kwenye cover lake tu itakuwa ‘unique’ kwa sababu ntakuwa nimekaa nimevalishwa shela, kuonesha kwamba ni kweli nimekubali kuolewa, hii itakuwa tofauti na movie nyingi nilizowahi kucheza, itakuwa ‘Unique’.” Dk Cheni aliiambia tovuti ya Times Fm.
Share on Google Plus

About MWERA AMAZING

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Post a Comment