Msanii toka nchini Kenya, Victoria Kimani, amefunguka
na kusema kuwa hana mausiano yoyote ya kimapenzi na msanii wa +255, Diamond
Platnumz, kufuatia tetesi zilizozagaa katika nchi hizi mbili kutokana na zile
picha walizokuwa wamepiga wakiwa nchini Afrika Kusini.........
“Sifahamu hizi tetesi zimetokea wapi. Nilikutana
na Diamond mara
moja, na ilikuwa wakati tunarekodi wimbo wa ONE Campaign Afrika Kusini wiki
mbili zilizopita.” .
Aliendelea kwa kusema kuwa “Hata sina namba yake, kwa
hiyo sijawasiliana nae tangu tulivyokutana Afrika Kusini.”
Lakini inasemekana kuwa Diamond alikanusha tokea
tetesi hizo zilivyoanza kushika chati katika masikio ya watu, alisema kuwa
hawana mausiano ya kimapenzi bali ni washikaji tu.
0 maoni:
Post a Comment