MWERA AMAZING BLOG

MWERA AMAZING BLOG

WAMISRI WANAOMTUSI EL-SISI WAONYWA.



 Wafuasi wamebeba picha ya El-Sisi
Wizara ya mambo ya ndani ya nchi ya Misri imesema kuwa inachunguza maneno yanayoandikwa kwenye mitandao ya kijamii yakiwa na kitambulisho, yaani "hashtag", yanayomtusi waziri wa ulinzi aliyestaafu ili kugombea urais, Field Marshall Abd-el-Fattah el-Sisi..................


Heshtegi hiyo ambayo tafsiri yake ni "mpigie kura kuwadi", imesambazwa kwenye Twitter zaidi ya mara 100-milioni na imependwa na watu zaidi ya 40,000 kwenye Facebook.

Inaarifiwa kuwa wizara ya mambo ya ndani ya Misri imesema itawakamata watu wanaoitumia sana heshtegi hiyo.

Maneno hayo piya yamekuwa yakichorwa kwenye kuta za mjini Cairo chini ya mabiramu ya picha za Bwana Sisi.

Field Marshall E-Sisi aliipindua serikali iliyochaguliwa kwa njia za kidemokrasi ya Mohamed Morsi wa Muslim Brotherhood mwezi Julai mwaka jana.
kutoka BBC.
Share on Google Plus

About MWERA AMAZING

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Post a Comment