MWERA AMAZING BLOG

MWERA AMAZING BLOG

HIKI NDICHO ALICHOKISEMA DUDUBAYA, BAADA YA TAARIFA ZA HAPO JANA ZA KUMKATA SIKIO MAMA YAKE MKUBWA




Hapo jana kulikuwa na uvumi wa msanii wa Hip Hop nchini Tanzania Dudubaya, amemkata sikio mama yake mkubwa, lakini msanii huyo alopohojiwa alikanusha na kuyasema haya…….


Dudubaya ameanza kwa kusema>>’Hizo taarifa Soud mimi mwenyewe nimekuja kuwasha simu jana saa 9 kwa sababu juzi nilikuwa nimekesha au sio sasa kuwasha simu ndio naambiwa bwana unatafutwa hivi na hivi lakini umezima simu kwa lipi taarifa kama hizo mimi mwenyewe nimezisikia kama unavyoniambia na kwenye mtandao’

‘Nimepokea pia simu kutoka nchi mbalimbali washkaji zangu wanavyoniambia mimi nipo Shinyanga kwenye biashara zangu mimi siwezi kuishi kwa kujificha kama digidigi mimi ninafahamika halafu cha kushangaza kama Polisi Mwanza karibu Mapolisi wote wana namba zangu na hakuna hata mmoja aliyenipigia’

‘Mimi  nikiwa na kesi Polisi huwa napigiwa simu bwana eeh kuna tukio hili na hili tunakutafuta na ninaenda sasa nashangaa sijapigiwa simu na sijui kama kuna kesi kituo gani wala nini sasa hivi vitu hata sivielewi unajua nini mimi nina wasi wasi hii inshu na ndugu zangu binafsi’
dudu
Mimi ndugu zangu nawajua vizuri hawa wa ukoo wangu na nilikua siwajui zamani wakati mimi nahit kwenye muziki mwaka 2000 nilikua nawajali,nikienda mkoa huu mkoa nawajali lakini nawapa kipaumbele cha juu kabisa lakini nilivyokuwa naenda Mwanza kipindi cha nyuma ndugu zangu walikua wanaongea maneno kibao Ooh Dudubaya hajajenga kwao Kisesa hajafanya hivi’

‘Mwisho wa siku nilisikitika nilivyoenda kujenga nyumba kwa ajili ya mama yangu mzazi self container ya vyumba vinne sasa nilishangaa ndugu zangu wamenuna wamekasirika na hakuna anayenipigia simu kuniambia labda hongera wakati kabla walikua wanaongea maneno mengi’

‘Imetoka pale wakatumwa watu kwenda kupiga picha pale nyumbani wakapeleka kwenye gazeti la sani Watanzania walishawahi kuona hilo gazeti liliandikwa Dudubaya amtelekeza Mama yake mzazi hivi na hivi lakini walishindwa kupiga hilo jingo lililo kwenye renta’

‘Nilipokuja kumuuliza Yule Mwandishi wa lile gazeti akanambia Dudu mimi sijafika hata kwenu kuja kupiga picha waliofanya hivyo walaumu ndugu zako na jamaa zako na mimi sijaenda hata kwenu nikawajua hao ndugu lakini nikawapotezea’

‘Nawajua hao ndugu hata kwenye hili suala wanajaribu kutengeneza vitu Fulani kuwa huyu kafanya hivi kumkata sikio mama yake mkubwa kama kunichafulia nionekane kwenye jamii nionekane namna gani lakini kama kuna kesi Polisi na kama mama yangu huyo mkubwa kasema twende Mahakaman tutaenda Mahakamani lakini kitu nachoamini Yule ni mama yangu mimi ni mwane hivyo’.

Share on Google Plus

About MWERA AMAZING

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Post a Comment