Taarifa kutoka nchini Nigeria, zinasema kuwa mamia ya
watu waliuawa katika shambulizi lililofanywa na kundi la wapiganaji wa Boko
Haram katika mpaka wa nchi hiyo na Cameroon siku ya Jumanne............
Katika mahojiano na BBC kiongozi mmoja wa eneo hilo,
Ahmed Zanna, alisema kuwa washukiwa walivamia mji wa Gamboru Ngala, katika
jimbo la Borno, na kuwaua takriban watu 300.
Inaarifiwa wapiganaji hao waliwafyatulia risasi watu
kiholela katika soko kuu la eneo hilo.
Mwandishi wa BBC nchini Nigeria
anasema ilikuwa vigumu kupata taarifa hizo mapema kwa sababu ya changamoto ya
mawasiliano katika jimbo hilo hasa kwa sababu
eneo hilo liko mbali sana.
Wakazi wa eneo hilo
wanasema kuwa walipata zaidi ya maiti miamoja kutokana na shambulizi hilo.
Kutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment