MWERA AMAZING BLOG

MWERA AMAZING BLOG

PUTIN, HATAKI KURA YA MAONI UKRAINE.



 
Katika hatua ambayo haikutarajiwa Rais wa Urusi, Vladimir Putin, ametoa wito kwa makundi yanayotaka kujitenga wanaounga mkono Urusi Kusini Mashariki mwa Ukraine waahirishe kura ya maoni ya Jumapili juu ya kutaka kujitenga kama hatua muhimu kuimarisha mashauriano ya amani kati ya 
 makundi yanayozozana nchini humo...........


Rais Putin alisema kuwa hatua hiyo itaimarisha mazingira ya kufanya mashauriano kati ya Serikali ya Ukraine na wale nchini wanaopendelea Urusi wanaotaka maeneo yao kujitenga na kuungana na Urusi.
 
Amesema kuwa uchaguzi wa Urais uliopangwa kufanywa Mei 25, ni hatua inayofaa.

Siku chache zilizopita Bwana Putin alitaja uwezekano wa kuwa na uchaguzi huo wa Urais kama upuzi mtupu. Lakini katika taarifa ya hivi sasa Bwana Putin amesema uchaguzi huo hautakuwa na maana iwapo raia wote wa Ukraine hawatahusishwa na kuwahakikishia jinsi haki zao zitakavyolindwa baada ya uchaguzi.
Share on Google Plus

About MWERA AMAZING

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Post a Comment