Israel imesema kuwa
itaendeleza mashambulizi yake katika ukanda wa Gaza
hadi pale kundi la wapiganaji wa Hamas litakapositisha kurusha makombora katika
maeneo ya taifa hilo...................
Waziri mkuu nchini Israel Benjamin Netanyahu amesema kuwa hakuna shinikizo zozote za kimataifa zitakazozuia taifa lake kutumia uwezo wake na kwa matamshi yake mwenyewe akasema kuwa hakuna shambulizi lolote la kigaidi katika Gaza lenye kinga.
Zaidi ya watu 110 wengi wao wakiwa raia wa Palestina wameuawa kufuatia mashambulizi ya siku nne yanayotekelezwa na Israel katika eneo la Gaza.
Alipoulizwa iwapo Israel ilikuwa inajiandaa kutuma jeshi la ardhini nchini Palestina ,bwana Netanyahu alijibu kuwa Israel inajiandaa kwa lolote lile.
kutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment