BABU TALE " KUZOMEWA KWA DIAMOND PLATNUMZ NI MPANGO" KIZURI CHAJIUZA KIBAYA CHAJITEMBEZA.
Meneja wa msanii wa muziki nchini Diamond Platnumz, Babu Tale, amefunguka kuhusu tukio la siku ya Fiesta Jijini Dar es salaam, baada ya msanii wake Diamond kuzomewa akiwa Jukwaani leaders Club...........
Aliyasema hayo Babu Tale kupitia kipindi cha XXL-Clouds fm, kwamba tukio hili halikuwatisha kwani walikuwa na Taarifa mapema kabla ata ya Tukio lenyewe kutokea, " tulimjenga Kisaikolojia kwahiyo ni sehemu ya kazi na mashabiki ingekuwa wanapiga kelele kama tumekosea show kweli, lakini sio, hvyo show ilikuwa sawa" hayo yalikuwa maneno ya Babu Tale.
Tunachokijua ni kwamba msanii wetu anafanya kazi vizuri tu, na kwasasa nguvu zetu tumeziweka kwenye kuzikusanya Tuzo za Chanell O na MTV, Sie sasa hivi tunasonga mbele, pia chema chauza kibaya chajitembeza.
0 maoni:
Post a Comment