Marekani
imewapongeza wananchi wa Burkina Faso na viongozi wao kwa kutia saini mkataba
utakao ongoza serikali ya mpito kuelekea serikali iliyochaguliwa kidemokrasia.....................
"Tunampongeza
Michel Kafando kwa kuapishwa kuwa rais wa mpito wa Burkina Faso
Tunampa
moyo Bwana Kafando kuendeleza kasi iliyoanza wiki mbili zilizopita na
kuwachagua watu watakaosaidia kuendesha serikali ya mpito ambao wamejitolea
kujenga serikali ya kiraia na kidemokrasia.
Tunayataka
majeshi ya Burkina Faso kuendelea na jukumu lao la msingi la kulinda mipaka ya
Burkina Faso na usalama wa raia wake. Pia kwa serikali ya mpito jukumu la
serikali ya kiraia ya mpito ni kuhakikisha maandalizi kabambe kwa ajili ya
uchaguzi wa kitaifa utakaofanyika mwezi Novemba 2015 kama ilivyoanishwa katika
katiba"imesema taarifa ya Ikulu ya Marekani".
Michel
Kafando,Rais wa serikali ya mpito Burkina Faso
Aliyekuwa
waziri wa mambo ya nje Burkina Faso Michel Kafando, ametajwa kuwa rais wa mpito
nchini humo.
Jitihada
zimekuwa zikiendelea nchini humo kumchagua kiongozi wa mpito kufuatia
kuidhinishwa hapo jana na jeshi na viongozi wa mashirika ya kiraia kwa mpango
wa mwaka mzima utakaohakikisha kufanyika uchaguzi.
Kafando
alikuwa mmoja kati ya watu wanne ambao wangechukua wadhifa huo, wakiwemo
waandishi wawili na msomi mmoja.
Viongozi
wa mashirika ya kiraia na wawakilishi wa jeshi walishughulika hadi usiku katika
mji wa Ouagadougou kuamua nani atachukua wadhifa huo wa rais wa mpito.
Kwa
mujibu wa makubaliano hayo ya mpito, ilikuwa ni lazima awe raia ambaye
hatogombea katika uchaguzi huo.
Mwishowe
walimchagua raia aliyependwa zaidi na jeshi, mwenye umri wa miaka 72 na waziri
wa mambo ya nje wa zamani Michel Kafando, Sasa ni lazima amchague waziri mkuu
ambaye anaweza kuwa raia au afisa wa jeshi kuongoza serikali ya watu 25 ya
mpito.
Kutoka
BBC
0 maoni:
Post a Comment