Miaka
13 baada ya majengo ya awali ya Kituo cha Biashara cha Kimataifa, WTO
kuharibiwa katika shambulio la kigaidi la Septemba 11, 2001, kituo hicho
kilichopo jijini New York kimefunguliwa kwa shughuli za biashara..................
Waajiriwa
katika kampuni kubwa ya uchapishaji ya Conde Nast wameanza kuingia katika jengo
hilo la One World Trade Centre lenye urefu wa ghorofa 104.
Kituo
cha One World Trade Centre chapita majengo yote katika mtaa wa Manhattan,
jijini New York
Jengo
hilo lenye thamani ya dola za Kimarekani bilioni 3.8 limechukua muda miaka nane
kulijenga na kwa sasa ndilo jengo refu kuliko yote nchini Marekani.
Limekodishwa
kwa asilimia 60% na taasisi ya serikali ya Marekani ya Utawala wa Huduma
imeingia mkataba wa kuchukua eneo la futi za mraba 275,000.
"Mwonekano
wa angani wa jiji la New York umerejea tena," anasema Patrick Foye,
mkurugenzi mtendaji wa Mamlaka ya Bandari, ambayo yanamiliki eneo hilo
lililorejeshewa hali yake.
Sehemu
ya kubarizi ghorofani mwa jengo la One WTC, jijini New York
Jengo
hilo lenye urefu wa mita 541 kwenda juu liko katikati ya eneo hili, ikiwemo
sehemu ya eneo la kumbukumbu la majengo ya zamani na makumbusho yaliyofunguliwa
mwaka huu.
Eneo
la kubarizi juu ya jengo hili hatimaye litakuwa wazi kwa matumizi ya umma.
Watu
wakipita kando ya jengo la WTC jijini New York
Jengo
hili la One World Trade Center kwa sasa linatawala anga la eneo la
Baadhi
ya watu wamezungumzia uzuri wa jengo hili.
Wafanyakazi
wapatao 170 wa kampuni ya Conde Nast watakuwa wamehamia katika jengo hili wiki
hii, fwakijaza ghorofa tano. Wafanyakazi wapatao 3,000 zaidi watajiunga na
wenzano ifikapo mapema mwaka 2015.
Mkurugenzi
mtendaji wa mamlaka ya bandari Bwana Foye ameongeza kuwa jengo hili ndilo
"jengo lenye usalama zaidi nchini Marekani".
TJ
Gottesdiener wa kampuni ya Skidmore, Owings & Merrill ambayo ilitoa mchoro
wa mwisho wa jengo hili amesema jengo hili limevuka mfumo wa majengo yaliyopo
jijini
New York na limejengwa na kuimarishwa kwa zege la chuma cha pua.
Eneo
la jengo hili la One WTC pia imekodishwa kwa kampuni ya matangazo ya Kids
Creative, GSA, na futi za mraba 191,000 zimekodishwa kwa kampuni ya China,
ambayo inajishughulisha na masuala ya biashara na utamaduni.
0 maoni:
Post a Comment