Ripoti
ya shirika la kimataifa la kutetea haki za binaadamu Human Rights Watch inasema
polisi katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kwa jumla wamewaua vijana wapatao
51 katika operesheni ya kupambana na uhalifu Kinshasa................
Watu
wengine 33 hawajulikani waliko tangu operesheni hiyo ilopewa jina
"Operation Likofi", ilioidhinishwa Kinshasa mwaka uliopita kufanyika.
Human
Rights Watch liliwahoji zaidi ya maafisa 100 wa polisi, watu walioshuhudia
nauaji hayo pamoja na jamaa wa waathiriwa.
Shirika
la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch, liliwahoji zaidi ya maafisa
100 wa polisi , walioshuhudia matukio pamoja na jamaa wa waathiriwa waliotoa
taarifa ya kile kilichosemekana kuwa mauaji ya kiholela.
Msemaji
wa shirika la hilo,(Anneke Van Woudenberg), alituhumu serikali kwa kuficha
taarifa kuhusu mauaji hayo na kusema familia za waathiriwa zilikuwa zimetishwa
na kuonywa dhidi ya kufichua taarifa za mauaji hayo.
Ripoti
iliyotolewa na umoja wa Mataifa mwaka jana pia ilielezea kuhusu mauaji hayo.
Kutoka
BBC
0 maoni:
Post a Comment