Baada
ya kushindwa vibaya kwa chama cha Democrat kwenye uchaguzi wa viti vya bunge la
seneti nchini marekani rais wa marekani Barack Obama amewakaribisha viongozi wa
baraza la congress kutoka vyama vyote katika ikulu ya white White House siku ya
ijumaa kujadili mwelekeo wa siasa za nchi hiyo...................
Kutoweza
kufanya kazi kwa pamoja baina ya rais na Congress kumezorotesha kupitishwa kwa
miswada na viongozi wa Republican.
Seneta
wa Republican na kiongozi wa walio wengi Mitch Mc Connell amepata tena kiti
chake katika jimbo la Kentucky.
Chama
cha Republican kimezoa viti vingi katika uchaguzi huo na kukifanya kuchukua
udhibiti wa taasisi hizo muhimu dhidi ya kile cha Democrat.
Kiongozi
wa zamani wa seneti kutoka chama cha Democratic , Harry Reid, amemuita
Mitch
McConnell kumpongeza na akasema ilikuwa ni wazi kwamba wapiga kura walitaka
vyama vyote kushirikiana.
Mwenyekiti
wa Kamati ya kitaifa ya Republican Reince Priebus amesema kuwa umma wa
wamarekani umekiamini chama chake.
Chanzo BBC
0 maoni:
Post a Comment