MWERA AMAZING BLOG

MWERA AMAZING BLOG

MAREKANI NA URUSI KUKUTANA GENEVA

Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani John Kerry, anapanga kukutana leo na Waziri mwenzake wa Urusi Sergey Viktorovich Lavrov, kando na mkutano unaoendelea wa umoja wa mataifa huko mjini...................


Geneva kuhusu ukiukaji wa haki za binadamu nchini humo.

Huu ndio utakuwa mkutano wao wa kwanza tangu Kerry amzome Lavrov kwa kudanganya kuhusu mchango wa Urusi katika mapigano yanayoendelea nchini Ukraine.

Mkutano huo vilevile unasadifiana na kutolewa kwa ripoti maalum ya Umoja wa mataifa inayoshtumu vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu mashariki mwa Ukraine.

UN inasema kuwa zaidi ya watu 6000 wameuawa tangu mapigano hayo yaanze huku mamia wakiuawa katika majuma machache yaliyopita.

Bwana Kerry anatarajia kuzua mjadala kuhusiana na mauaji ya kiongozi wa upinzani ambaye pia ni mpinzani sugu wa rais Putin Boris Nemtsov
Kiongozi huyo alipigwa risasi na kuuawa karibu na makao makuu ya urais wa urusi Kremlin siku ya ijumaa iliyopita.
Huku hayo yakijiri, Tume ya jumuia ya Bara Ulaya inatazamia kufanya mazungumzo kati ya Moscow na Kiev, ili kutazua tatizo lililoko kuhusiana na usambazaji wa gesi.

Juma lililopita kampuni kubwa ya uuzaji gesi, Gazprom, liliwaonya wasambazaji wake kuwa itakomesha pakubwa uuzaji wake wa gesi nchini Ukraine hadi Ukraine kutuma malipo yake ya gesi mwezi huu wa Machi.

Aidha mataifa hayo mawili yanatofautiana kuhusiana na usambazaji wa awali wa gesi kwa makundi ya wapiganaji mashariki mwa Ukraine.

Mwezi uliopita, Kiev ilisimamisha kutuma gesi hadi katika maeneo yaliyojitenga, ikidai kuwa mabomba ya kupitishia mafuta na gesi yameharibiwa huku kampuni ya Gazprom ikiwasambazia waasi mafuta moja kwa moja.
kutoka BBC
Share on Google Plus

About MWERA AMAZING

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Post a Comment