Ndege ya abiria
inayomilikiwa na shirika la ndege la Germanwing Airbus A320 Imeanguka katika
milima ya Alps nchini Ufaransa..............
Ndege hiyo ilikuwa
imewabeba abiria 142 na wahudumu 6 ikitoka Barcelona Uhispania kuelekea
Duesseldorf.
Ndege hiyo
inayomilikiwa na shirika la ndege la Ujerumani Lufthansa chini ya nembo
Germanwings imeripotiwa kuanguka karibu na mji wa Digne.
Ndege hiyo ya A320
ilianguka saa tano asubuhi katika Kusini mwa Milima ya Alps.
Viongozi wa Ujerumani
na Ufaransa wanaendelea kushauriana kuhusiana na mkasa huo unaowakabilia macho.
Ndege hiyo ya Ujerumani
ilianguka katika eneo lisilo na mijengo ambalo halifikiki kwa urahisi nchini
Ufaransa Kusini mwa Milima ya Alps.
Rais wa Ufaransa
Francois Hollande ametaja ajali hiyo kama mkasa na amesema kuwa uwezekano wa
kuwapata watu wakiwa hai ni mgumu.
Hali ya hewa katika
eneo hilo ilitajwa kuwa nzuri na kituo maalumu cha kukabiliana na mikasa
kimetengwa kukabiliana na mkasa huo.
Waziri wa Maswala ya
ndani ya nchi uko njiani kuelekea mahali pa ajali hiyo.
Vyombo vya habari
nchini Ufaransa vinasema kuwa ndege hiyo ilituma ujumbe wa kuwa hatarini kabla
ya mawasiliano yake kutoweka .
kutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment