Jack Warner amesema
atafichua kila anachojua katika FIFA
Aliyekuwa makamu wa
rais wa shirikisho la soka duniani FIFA Jack Warner amesema katika hotuba ya
kushangaza aliyotoa katika runinga kwamba atafichua kila anachojua kuhusu
ufisadi katika shirikisho hilo.............
Bwana Warner ambaye
alisema kuwa anahofia maisha yake pia amesema kuwa anaweza kuwahusisha maafisa
wa FIFA na uchaguzi mkuu katika taifa la Trinidad and Tobbago mwaka 2010.
Maafisa wa FIFA
wanaotuhumiwa na ufisadi
Ni mmoja wa watu 14
walioshtakiwa na Marekani kuhusiana na ufisadi katika FIFA.
Mmoja wa maafisa wakuu
wa FIFA na shahidi muhimu Chuck Blazer alikubali kuchukua hongo.
Chuck Balzer akiwa na
Sepp Blatter
Afisa huyo alikiri
kufanya hivyo mnamo mwaka 2013,ikiwa ni miongoni mwa mashtaka yaliofunguliwa
ambayo yameikabili FIFA na kumlazimu rais wake Sepp Blatter Kujiuzulu.
Idara ya mahakama ya
Marekani inadai kuwa watu 14 walioshtakiwa walikubali hongo ya zaidi ya dola
milioni 150 katika kipindi cha miaka 24.
Chuck Blazer amekiri
kupokea hongo
Watu wengine wanne
walikuwa tayari wameshtakiwa akiwemo Blazer
chanzo BBC
0 maoni:
Post a Comment