Maafisa wa serikali Kaskazini mwa Nigeria
wamesema kuwa watu 25 wameuawa katika shambulio la bomu la kujitolea mhanga
katika mji wa Zaria...........
Ripoti
zinasema kuwa watu wengine 32 wamejeruhiwa kwenye shambulizi hilo.
Shambulio
hilo lilitokea katika jengo moja la serikali ambako wafanyakazi wa serikali
walikuwa wamekusanyika kusajiliwa.
Wengi
waliokuweko ni walimu na wafanyikazi wa umma.
Katika
kipindi cha majuma 2 yaliopita takriban watu 220 wameuawa katika mashambulizi
kadha yanayolaumiwa kutekelezwa na kundi la wapiganaji wa Boko Haram.
Gavan
wa jimbo la Kaduna amewaonya wenyeji kuwa waangalifu sana na kuepuka maeneo
yaliyojaa watu kwani hayo ndio yanayolengwa na washambuliaji wa kujitolea
mhanga.
Gavana
Nasir El-Rufa'I amewasihi wenyeji waepuke misikiti makanisa masoko na vituo vya
mabasi hadi pale hali itakapotulia.
Inspekta
wa polisi wa Nigeria ameomba wanigeria kuwa makini na waangalifu akisema kuwa
''kwa sasa inaonekana mabomu yameundwa mengi na kwa hakika likishaundwa bomu ni
vigumu sana kuzuia mashambulizi ya kujilipua kwenye umati wa watu ilikuzidisha
maafa''.
Tayari
hofu imetanda katika mji wa Abuja ambapo Polisi wamepiga marufuku uuzaji na
uchuuzi katika barabara za katikati ya mji.
kutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment