Kundi la Islamic State
nchini Syria limeteka vijiji kadhaa kutoka katika makundi hasimu ya wapiganaji
kaskazini mwa mji wa Aleppo licha ya mashambulizi ya angani kutoka kwa jeshi la
Urusi, ambapo Moscow inasema ilikuwa ikilenga kundi hilo.
Mwandishi wa BBC katika
eneo hilo amesema kuwa licha ya madai ya Urusi kwamba inawalenga wapiganaji wa
IS,Inaonekana kwamba kuyalenga makundi mengine ya waasi ambayo ni tishio kwa
serikali ya Syria ambayo inaungwa mkono na Mascow.
Anasema kuwa kampeni ya
mabomu inayotekelezwa na Urusi imeyadhoofisha makundi hayo na hivyobasi kutoa
fursa kwa IS kusonga mbele.Wakati huohuo Kamanda mmoja mkuu wa walinzi wa
kikosi cha mapinduzi nchini Iran, ameuwawa, baada ya kwenda kuwapa ushauri
wanajeshi katika harakati zao za kukabiliana na kundi la Islamic State nchini
Syria.
Iran inasema kuwa
Jenerali Hussein Hamedani aliuwawa siku ya Alhamisi wakati wa ujumbe wa ushauri
kaskazini mwa mji wa Aleppo.
Jenerali Hamedani
alijadiliwa katika vikwazo vya jumuia ya bara Ulaya dhidi ya baadhi ya viongozi
wa Iran baada ya kuhusika katika kuukandamiza upinzani baada ya matokeo tata ya
uchaguzi wa Urais uliofanyika mnamo mwaka 2009.
Ni miongoni mwa
makamanda wa jeshi wa Iran ambao wameuwawa huko.
Iran imekuwa ikiisaidia
pakubwa utawala wa Rais Asaad wa Syria, tangu mapigano ya wenyewe kwa wenewe
yalipoanza.
chanzo BBC
0 maoni:
Post a Comment