Maduka ya jumla ya
Uchumi yametangaza kufungwa kwa oparesheni zake nchini Tanzania na Uganda
katika zoezi la kubana matumizi .
Mkurugenzi mkuu wa
maduka hayo Dr.Julius Kipng'etich amesema kuwa bodi yake imeamua kufunga vituo
hivyo kwa lengo la kutathmini muundo wa oparesheni zake nchini Kenya. ''Maduka
yetu nchini Tanzania na Uganda yanajumlisha asilimia 4.75 ya oparesheni zetu
licha ya kutugharimu asilimia 25 ya oparesheni zetu''.
Maduka ya uchumi katika
mataifa hayo mawili hayajazalisha faida yoyote katika kipindi cha miaka 5 swala
ambalo linalazimu faida zinazopatikana katika maduka ya Kenya kutumika,alisema
Kipng'etich.
Mkurugenzi huyo amesema
kuwa tayari maduka hayo yameandika barua kwa Mamlaka ya masoko nchini Kenya
,soko la hisa pamoja na washikadau muhimu kuhusu uamuzi huo na kuongezea kwamba
hivi karibuni uchumi itahitaji kuungwa mkono na wamiliki wa hisa ili
kuidhinisha mpango huo.
Maduka yote katika
mataifa hayo mawili yamefungwa.
Chanzo ni BBC Swahili.
0 maoni:
Post a Comment