Picha hizo zinaonesha
kuwa zilipigwa katika chuo cha kiufundi cha Bama (Government Technical College
Bama (GTCB)
Kundi la wapiganaji wa
Kiislamu la Boko Haram wamezindua kiwanda wanachotumia kuunda mabomu na silaha
zingine kali Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.
Picha hizo zilitumwa
kwa idhaa ya Hausa ya BBC kupitia kwa namba iliyosajiliwa nchini Cameroon.
Kupitia kwa mtandao wa
WhatsApp picha hizo zilitumwa kwa idhaa ya Hausa ya BBC kupitia kwa namba
iliyosajiliwa nchini Cameroon.
Wapiganaji hao wakipaka
rangi silaha zao
Picha hizo zinaonesha
watu wanaoaminika kuwa wafuasi wa kundi hilo wakiwa kwenye karakana fulani
wakitengeneza silaha zenye uwezo wa kufanya uharibifu mkubwa.
Picha hizo zinaaminika
kuwa zilipigwa katika jimbo la Borno nchini Nigeria.
Wachunguzi wanasema
kuwa picha hizo zinaonesha kuwa zilipigwa katika chuo cha kiufundi cha Bama
(Government Technical College Bama (GTCB).
Haijabainika iwapo
mashine hizo za chuo hicho anuai zilinaswa na maafisa wa jeshi la Nigeria au
la.
Hata hivyo Bama ni moja
ya miji iliyokombolewa na jeshi la Nigeria.
Sehemu ya kwanza ya
mifereji ikikatwa kutengeneza silaha
Licha ya waasi hao
kupigwa na kuondolewa katika maeneo mengi ya kaskazini mwa Nigeria kundi hilo
limeendelea kufanya mashambulizi ambayo yamewaacha wa Nigeria wengi wakishangaa
wanakotoa silaha hizo kali.
Huu ndio ushahidi wa
kwanza kuwa kundi hilo linauwezo wa kutengeneza silaha kali.
Huu ndio ushahidi wa
kwanza kuwa kundi hilo linauwezo wa kutengeneza silaha kali.
kutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment