Rais Jakaya Mrisho
Kikwete wa Tanzania amefanya mazungumzo na makamu wa rais wa kwanza kisiwani
Zanzibar ambaye ndiye mgombea Urais kupitia tiketi ya chama cha upinzani (CUF)
Maalim Seif katika Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Hatua hiyo inajiri
wakati ambapo kuna mkwamo wa kisiasa kisiwani humo baada ya Tume ya
Uchaguzi(ZEC) kufuta matokeo ya uchaguzi uliofanyika .
Hatahivyo mwandishi
wetu aliyezungumza na mkurugenzi wa maswala ya mawasiliano katika chama cha CUF
amesema kuwa hakuna lolote la muhimu lililoafikiwa isipokuwa 'mazungumzo ya
kawaida'.
Amesema kuwa
wamehuzunika baada ya kubaini kuwa rais Jakaya Kikwete anakamilisha muhula wake
wa uongozi hapo kesho
0 maoni:
Post a Comment