Somalia
imetangaza kuvunja uhusiano wa kidiplomasia na Iran ikiituhumu kwa kuingilia
masuala ya ndani ya Somalia.
Serikali ya
Somalia imewapa maafisa wote wa ubalozi wa Iran mjini
Mogadishu muda wa saa 72
(siku tatu) wawe wameondoka nchini humo.
Uamuzi huo
umechukuliwa baada ya mkutano wa baraza la mawaziri wa Somalia.
“Hatua hii
imechukuliwa baada ya kutathminiwa kwa kina na kutokana na hatua ya Jamhuri ya
Iran kuendelea kuingilia masuala ya ndani ya Somalia,” taarifa kutoka wizara ya
mashauri ya kigeni ya Somalia imesema.
"Jamhuri ya
Somalia inaitaka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuheshimu uhuru wa mataifa yote
kwa mujibu wa sheria za kimataifa, Mkataba wa Vienna kuhusu Uhusiano wa
Kidiplomasia wa mwaka 1961 na tamaduni za uhusiano wa kidiplomasia.”
Kutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment