Idris Sulutan, mshindi
wa Big Brother Africa, usiku wa kuamkia leo amepost ujumbe wa uzuni baada ya
aliyekuwa mpenzi wake Wema Sepetu, inadaiwa kuwa alikuwa mjamzito lakini mimba
yake iliweza kutoka kabla ya siku.
Idris alipost picha ya
watoto mapacha na kuandika ujumbe huu “Ni haraka
sana mmeingia katika mfumo wa maisha yetu, lakini ni haraka pia mmetuacha,
sikuwahi kupata nafasi ya kukutana na nyinyi, nina vingi nataka niseme
ninavyofikiria ndani ya kichwa changu vinatosha kunifanya mwendawazimu,
ukizingatia mmeishi kwa wiki sita pekee, tuliwapenda sana na natamani ningepata
nafasi ya kuwashika, mungu ametoa na mungu ametwa kama ambavyo amepanga na
hatuwezi kulalamika huenda ametuandalia mengine mazuri zaidi”
0 maoni:
Post a Comment